Denti Shouts

1. TeeZee Nation-Taifa la vipaji, Inakuletea

“Denti Shouts- Shout for Knowledge”. Kupitia www.winksite.mobi/dentishouts/tz

2. Denti-Shouts: Ni nini?

Huu ni mtandao jamii,uliobuniwa na Lazaro.K.Mawe,Unaopatikana kwa njia ya intaneti,kwa kupitia simu ya mkononi au komputa,Mtandao huu si wa kulipia,ni bure kujiunga.Faida za muanachama atakaye jiunga .

 Kutengeneza wasifu wenye picha
 Kupata habari mabimbali zinazolenga kuboresha maisha ya mwanafunzi wa kitanzania kama vile afya ya uzazi,Elimu ,michezo,Utamaduni,Historia n,k
 Kuchangia habari/hadithi kwenye kijarida/ukurasa
 Kushiriki mijadala
 Kukutana/kupata marafiki wapya
 Kuchati
 Kupata ratiba ya matukio mbalimbali
 Habari na viunganishi vya tovuti zingine

3. Kazi za Denti-Shouts ni zipi?

• Kazi yetu ni kukusanya habari/taarifa muhimu kilingana na maoni mbalimbali ya wadau wanaojishughulisha na mambo yanayohusu elimu hasa ya hapa kwetu Tanzania,ikiwemo wazazi,walimu,asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali na wanafunzi kisha kuziweka katika tuvuti hii/mtandao ili jamii husika iweze kuzipata kirahisi zaidi.

• Kuandaa matamasha/mashindano yanayowahusu wanafunzi kulingana na ngazi yao,kupitia matamasha haya tunaamini kuwa hii ni njia rahisi zaidi ya kuwakutanisha wanafunzi kufurahia pamoja na kubadilishana uzoefu walionayo kiutamaduni kielimu na kijamii na pia kujenga urafiki na kudumisha amani ya nchi yetu.

KUHUSU SHINDANO

1. Jina La Shindano

“NAPENDA MICHEZO”

Hili ni shindano la uandishi wa insha,linalomtaka mwanafunzi aandike insha isiyopungua maneno 250 na isiyozidi maneno 350,akieleza ni kwa jinsi gani kijana anaweza kuleta maendeleo kwake na kwa mazingira yaliyo mzinguka. (Mfano; Mtaa, Kata, wilaya, mkoa au nchi)

2. Masharti ya Shindano

• Sindano linahusisha Shule kumi (10) katika mkoa/wilaya na litadumu kwa muda wa mwezi mmoja.
• Mwanafunzi natakiwa atumie mchezo anapoupenda kuelezea jinsi gani yeye au jamii anayomzunguka inaweza kufaidika,na kwa jinsi gani?ni vikwazo gani anakutananavyo na mfano wa mwanamichezo anayemvutia.
• Katika wiki ya kwanza ya shindano shule zinazoshiriki zinapaswa kushindanisha wanafunzi wake ili kupata mshindi mmoja atakaye wakilisha shule yake katika mchuano wa wanafunzi kumi (10) bora.
• Katika wiki ya pili washindi kumi (10) watatakiwa kuchuana ili kupata insha tano (5) bora.
• Shindano hili la uandishi wa insha linahusu wanafunzi wa kidato cha tatu na cha nne.

3. Jinsi ya Kushiriki

 Mshiriki unatakiwa kusoma maelezo juu ya shindano na kuyaelewa kabla ya kushiriki.
 Jiandikishe jina lako katika orodha ya washiriki wa shindano hili shuleni kwako.
 Andika insha ukifuata vigezo na masharti
 Kusanya Insha yako kwa mwalimu husika,kabla ya tarehe ya mwisho
 Subiri matokeo

4. Vigezo vya kumpta mshindi

• Alama za mwalimu
• Kura za Wanafunzi
• Kura kwa njia ya simu/ujumbe mfupi
• Barua/barua pepe
• Maoni kupitia mtandao wetu/facebook

MUUNDO/RATIBA YA SHINDANO

 Wiki ya kwanza
Jumamosi/Novemba 5-2011
Uzinduzi wa shindano kwenye kipindi cha redio (CG FM-Radio),
Jumatatu/Novemba 7,
Usambazaji wa vipeperushi ma matangazo mashuleni/na maeneo ya wadau wa elimu,
Jumanne/Novemba 8 hadi Ijumaa Novemba 11,
Kuelezea shindano katika shule husika ili kuwapa wanafunzi ufahamu juu ya shindano na jinsi ya kushiriki

 Wiki ya pili,
Jumamosi/Novemba 12-2011
Kutangazwa Kwa kuanzwa rasmi Kwa shindano (CG FM-Radio, Tabora)
Jumatatu/Novemba 14-hadi Jumatano 16-2011
Uandishi wa insha na ukusanyaji
Alhamisi /November 17-Hadi Ijumaa 18
Usahishaji wa insha.

 Wiki ya tatu
Jumamosi/Novemba 19-2011
Kutangazwa Kwa washindi kumi, kila shule kupata mshindi mmoja (CG FM Radio)
Jumatatu/Novemba 21- Hadi Ijumaa 25,
Ukusanyaji wa Alama za walimu, maoni ya wadau, ne Kura za wanafunzi kupitia njia zetu za ukusanyaji maoni kama zilivyoolodheshwa.

 Wiki ya nne
Jumamosi/November 26-2011
Kutangazwa kwa washindi watano bora (CG FM Radio)
Sherehe fupi ya kutoa zawadi, washiriki wote na wanafunzi watakaribishwa kushiriki

KWA KUANZA-SHINDANO LA KWANZA LITAFANYIKA MKOANI TABORA
(TANZANIA-NOVEMBA 2011)

***MWISHO***

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: